Katika kusheherekea miaka 23 ya ndoa yao mwanasoka mkongwe David Beckham na mkewe Victoria Beckham wamerudia upya viapo vyao vya ndoa wakiwa mapumzikoni nchini Ufaransa.
Wawili hao walirudia upya viapo hivyo mbele ya mnara maarufu duniani wa Eiffel Tower ulioko jijini Paris siku ya Jumatatu.
Siku ya Jumanne walionekana wakijivinjari katika jiji hilo la mapenzi huku wakiwa wamevalia nguo zenye rangi zinazofanana.
“Leo tunasherehekea miaka 23 ya ndoa yetu. David wewe ni kila kitu kwangu, ninakupenda sana!!!! ????” aliandika Victoria.
Kwa upande wake Beckha aliweka kipande cha video cha sekunde 90 na kuandika; “Miaka 23 iliyopita Posh ulianza kuwa mke wa Beckham, utaendelea kuwa Posh ❤️,” aliandika Beckham na kuwa-tag mkewe na watoto wao wanne.
“Heri ya miaka 23 ya ndoa yetu WOW miaka 23 & na watoto 4, watoto wazuri ❤️❤️❤️❤️ Ninawapenda , sote tunawapenda ❤️.”