Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Batuli: Queen wa Dr. Mwaka asaidiwe

Mke Wa Dk Mwaka Msdf Batuli: Queen wa Dr. Mwaka asaidiwe

Wed, 8 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwigizaji na mama wa watoto wawili, Batuli amesema kuwa mke wa mtaalam wa tiba asilia na mfanyabiashara maarufu nchini, Juma Mwaka ‘Dr. Mwaka’ anayejulikana kama Queen anapaswa kupewa msaada badala ya kuzomewa na kubezwa kama ambavyo baadhi ya watu wanamdhihaki mtandaoni.

Batuli amesema hayo baada ya sakata la Queen kuomba talaka ili aachane na mumewe Dr. Mwaka kwa akile alichodai kuwa amechoka na manyanyaso ndani ya ndoa yake hiyo aliyoishi kwa miaka 10.

“Tumezoea kusubiri mtu afe ndio tutafute cha kuongea, wanawake wengi tunaishi na wenza wetu ili watu watuone tupo kwenye maisha ya ndoa ila ukweli ni kwamba wengi wetu ni watumwa na tunaishi aidha kwa kulea watoto wakue au siku ziende kifo kifike tuondoke huo ndio ukweli wa 100%.

“Machozi, maumivu, mateso na unyanyasaji ndio vimejaa kwenye ndoa nyingi sana na akisimama mwanamke mmoja kama huyu basi anaonekana hana uvumilivu na kubezwa juu na ukikaa kimya na kukubali haya kifo chako ndio kinakuja kuongea, mbaya zaidi akitokea au wakitokea wanaume kusimama na wewe watachafuliwa kwa hali na mali ili tu uendelee kuishi kwenye jahanam ya dunia.

“wanawake wenzangu hakuna neno nimetoka nae mbali au nimechuma nae mali acheni utumwa wa akili na upofu wa mali, furaha huna, amani huna yaani duniani haupo na akhera unauliziwa, amkeni na mjipiganie kisha msaada utakukuta mbele kwa mbele. Huyu dada anahitaji msaada mkubwa sana sio kubezwa wala kuzomewa kifupi huyu ni shujaa haswa Queen,” amesema Batuli.

Queen ambaye anajishughulisha na utengenezaji wa keki, imeelezwa yeye na Dr. Mwaka wameishi pamoja takribani miaka 10 huku wakiwa wamejaaliwa watoto wawili.

Queen amesema kwa hatua aliyofikia mali sio muhimu kwake bali anataka talaka yake awe na maisha yake mengine yenye amani badala ya vitisho na kukosa uhuru juu ya maisha yake hata hivyo Dr. Mwaka anaonekan ahayupo tayari kutoa talaka sababu haijawa wazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live