Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashungwa Amjulia Hali Mzee King Kikii

Bashungwa Kingkikii?fit=1096%2C731&ssl=1 Bashungwa Amjulia Hali Mzee King Kikii

Mon, 24 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amehimiza Wasanii nchini kuhakikisha wanamiliki Bima za Afya ambazo zitawasaidia wanapokua wagonjwa wakati wowote.

Mhe. Bashungwa amesema hayo alipomtembelea Msanii Mkongwe wa Mziki wa Dansi nchini Kikumbi M. Mpango maarufu King Kikii Nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam Mei 22, 2021.

“Wizara itaendelea kufuatilia kwa ukaribu matibabu yako na kwasababu daktari wako tuna mawasiliano ya karibu tutakuwa tunajua hali yako inavyoendelea kila siku” alisisitiza Mhe. Bashungwa.

Kwa upande wake Msanii King Kikii amemshukuru Waziri Bashungwa kwa kumtembelea na kumfariji pia amemuomba Waziri amfikishie Salam zake kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuliongoza Taifa.

Mzee King Kikii ametumia nafasi hiyo kuwaasa wanamziki na wasanii wengine kuwa na nidhamu katika kazi ili kuendelea kufanya sanaa kwa muda mrefu.

Chanzo: globalpublishers.co.tz