Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basata yasitisha matamasha na burudani kwa siku 14

11896 BASATA+PIC Basata yasitisha matamasha na burudani kwa siku 14

Fri, 19 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Dar es Salaam. Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) limetangaza kusitisha matamasha na burudani kwa siku 14 kutokana na msiba wa aliyekuw Rais wa Tanzania, John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.

Taarifa iliyotolewa na kaimu katibu mtendaji wa Basata, Matiko Mniko inasema baraza limewaelekeza wadau wake kusitisha vibali vya matamasha na burudani kwa siku 14 ili wananchi waungane kuomboleza msiba wa Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli

“Baraza limewaelekeza wadau wake kusitisha vibali vya matamasha na burudani kwa siku 14 kuanzia Machi 17 ili wananchi waungane kuomboleza katika kipindi hiki kigumu kwa Taifa,” imesema taarifa hiyo.

Rais Magufuli alifariki dunia juzi Jumatano Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Akitangaza msiba huo, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alisema Rais Magufuli alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo.

Related



Mwili wa Magufuli kuagwa mikoa minne
Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz