Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basata wampongeza Diamond tuzo za Afrimma

Diamond Kusuka Basata wampongeza Diamond tuzo za Afrimma

Mon, 26 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Sanaa la Taifa limempongeza Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na wasanii wengine kutoka Bongo ambao wameteuliwa kuwania tuzo za Afrimma 2022.

Kupitia ukurasa rasmi wa Basata wameweka pongezi zao na kuanisha wasanii wanaowania tuzo hizo kama ifuatavyo:

BEST MALE EAST AFRICA 1.Diamond Platnumz 2.Rayvanny

ARTIST OF THE YEAR 1.Diamond Platnumz

BEST LIVE ACT. 1.Diamond Platnumz 2.BARNABA

BEST COLLABORATION 1.Diamond Platnumz 2.Marioo 3.Loui

VIDEO OF THE YEAR 1.Diamond Platnumz 2.Mbosso

ALBUM OF THE YEAR 1.Diamond Platnumz

BEST FEMALE EAST AFRICA 1.ZUCHU 2.MAUA SAMA 3.NANDY

“Majina ya wateule hawa yaliwekwa hadharani Septemba 14, 2022 katika mtandao wa Afrima, ni wazi kwamba Tanzania inazidi kupaa zaidi kimataifa kupitia fani ya Muziki.

Hivyo basi Watanzania tujitokeze kwa wingi kuwapigia kura wateule wetu hawa ili waweze kushinda Tuzo hizi za AFRIMA 2022.

Tuzo za Muziki Afrika (AFRIMA) Ni tukio la kila mwaka la utoaji tuzo. Tuzo hizi zilianzishwa na kamati ya kimataifa ya AFRIMA, wakishirikiana na umoja wa Afrika (AU) kwa ajili ya kutunza na kuwapongeza wasanii, vipaji na ubunifu katika bara la Afrika lakini pia kusambaza na kukuza urithi na utamaduni wa Afrika, onyesho lake la tuzo za waanzillishi lilifanyika mnamo 2014,” waliandika Basata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live