Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Basata, TCRA, Bakita na Polisi kuwafunda maadili wasanii

Basata Pic Data.png Basata, TCRA, Bakita na Polisi kuwafunda maadili wasanii

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Siku moja baada ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Pauline  Gakul, kufanya ziara Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na kuonyesha kukwazwa na kiki zinazoendelea kwa wasanii, baraza hilo laitisha jukwaa la kutoa mafunzo ya maadili. Katika ziara hiyo, Waziri Gekul pamoja na mambo mengine aliyohoji kuhusu mahudhurio ya wasanii katika jukwaa la wasanii ambalo utaratibu wake ulikuwa kufanyika kila Jumatatu. Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Matiko Mniko katika majibu yake alisema huwa hawahudhuirii ambapo Waziri alihoji kama kuna faini kwa yeyote ambaye haendi wakiwemo hao wanaoongoza kwenda kinyume na maadili. Hata hivyo leo Jumanne Aprili 27, 2021 kwenye ukurasa wao Basata waliandika kuwepo kwa Jukwaa la Sanaa siku ya Alhamini na kueleza  mada itahusu Maadili katika Sanaa. Katika jukwaa hilo watoa mada wanatarajiwa kutoka Basata, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Baraza la Kiswahili Tanzania (Bakita) na Jeshi la Polisi na litafanyika ukumbi wa Nafasi Art Space Mikocheni jijini Dar es Salaam. Jana katika ziara hiyo ya  Waziri Gekul, alionekana kukerwa na masuala ya kiki yanayoendelea na kueleza kuwa watanzania pamoja na serikali hawafurahishwi na wanakwazwa watu huku akitaka Basata kukaza uzi katika kuwapa adhabu kali bialy a kuwaonea haya. “Hivi ni lazima kuleta mambo yako binafsi ya mahusiano kwa umma kwamba umezaa na huyu, una orodha ya mademu kadhaa umetembea nao, inadhalilisha utamaduni wetu na kutuharibia kizazi chetu na kuona ni fasheni . “Mnatuharibia kizazi chetu, inafika mahali hadi mtoto anadhalilishwa na kuongelewa siku nzima mtoto ni zawadi kutoka kwa Mungu ni Baraka, kwa kweli inaumiza, Basata kaeni na hao wasanii muwaeleze haturidhishwi na hayo mambo ukizingatia kuna wasanii hawaelezi hayo mambo yao binafsi lakini wanafanya vizuri tu kwenye Sanaa yao,” amesema Waziri huyo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz