Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barnaba awakutanisha Diamond na Kiba

KIBA MONDI BARNABA Barnaba awakutanisha Diamond na Kiba

Tue, 16 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Barnaba Boy; ni mwanamuziki aliyekamilika wa Bongo Fleva ambaye anasema kuwa, Agosti 16, 2022 ni siku kubwa mno kwake kwani anakwenda kuachia albam yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Love Sounds Different.

Barnaba anakiri kwamba ndani ya albam hiyo kuna Ngoma ya Cheketua Acoustic Remix ambayo amemshirkisha King Kiba ambaye ni mshikaji wake mkubwa.

Habari za uhakika zinasema kuwa pia ndani ya albam hiyo kuna ngoma ambayo amefanya na Diamond Platnumz na Focalist wa Afrika Kusini hivyo wote watapatikana ndani yake.

Barnaba anakiri kuwaalika wawili hao huku pia akikiri kupata sapoti kubwa kutoka kwa Diamond ambaye amejitoa kimasomaso kama executive producer wa albam hiyo ambayo amekuwa akiifanyia promosheni ya kutosha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live