Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barnaba 'asusa' ampa Marioo Tuzo yake

Barnaba TMA Barnaba ampa Marioo Tuzo yake

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii Wa Bongo Fleva @barnabaclassic Amemjibu @marioo_tz baada ya kudai kuwa albamu iliyoshinda tuzo ya albamu bora mwaka 2023 [ Love Sounds Different ] ina nyimbo moja au mbili tu zilizo-hit, huku akidai kuwa aliandika moja ya nyimbo hizo.

Barnaba ameamua Kumjibu Marioo kuwa amekubali maneno yake na ameamua kumpa tuzo hiyo kwa moyo mmoja, akisema anastahili na kuanzia sasa tuzo hiyo itakuwa ya Marioo.

Hivi karibuni, Marioo alidai kuna fitna katika mchakato wa utoaji wa tuzo, akisisitiza kuwa haina maana kupokea tuzo ambayo mtu hajastahili. Aliwaomba waandaaji kujitathmini na kujipanga upya ili kuhakikisha haki inatendeka na kuhoji kwa nini waandaaji wanatoa tuzo zisizo na haki na kushirikisha washindani katika kutoa ushauri.

“Nawauliza waandaaji wa hizi tuzo, kwa nini mnatoa tuzo kama hazitendi haki? Mnaombaje ushauri kuhusu tuzo kwa wanaoshindania tuzo hizo hizo?………That was not fair at all. Inasikitisha na inakatisha tamaa. This time around jipangeni”. - Marioo Kupitia Ukurasa Wake Wa IG Story

Chanzo: www.tanzaniaweb.live