Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barnaba aitikia wito BASATA

Barnaba 1884 Barnaba akiwa Basata

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongofleva, Elias Barnabas almaarufu Barnaba ameitikia wito na kufika katika ofisi za BASATA Mei 9, 2024, lengo la wito huo ikiwa ni kujadili suala zima la maadili kutokana na msanii huyo kupandisha picha ambazo zilileta utata katika mitandao ya kijamii akiwa na msanii Yammi.

Aidha msanii huyo ameomba radhi kutokana na picha hizo na kuahidi kufuata utaratibu katika kulinda maadili mema ya nchi.

Pia Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji na Maendeleo ya Sanaa -BASATA, Edward Buganga amekabidhi msanii huyo kitabu cha Mwongozo wa Maadili katika kazi za sanaa na kutoa wito kwa wasanii nchini kuzingatia maadili katika kazi zao lengo ikiwa ni kujenga jamii yenye maadili mema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live