Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barnaba afunguka ishu ya kujiunga na WCB

Barnaba Na Diamonddd Barnaba afunguka ishu ya kujiunga na WCB

Sun, 14 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fundi wa muziki, Elius Barnaba amefunguka kuhusu suala la yeye kujiunga na lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) kwa kusema, hawezi kujiunga badala yake atashirikiana na bosi wa WCB Diamond Platnumz kuinua vijana wengine kwenye muziki.

Barnaba ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Agosti 13, 2022 alipokuwa anarejea nchini akitokea Sauz alipoalikwa na Diamond kwa ajili ya kumpa connection mbalimbali za kimuziki kuelekea kwenye uzinduzi wa albamu yake inayokwenda kwa jina la Love Sounds Different.

“Kwanza namshukuru sana Diamond kwa kujitoa kwake, kunisaidia hata kama ni kwa muda mchache kiasi gani lakini kwangu ina maana kubwa sana.

“Kuhusu kujiunga na WCB kwa sasa na kwa levo niliyonayo nadhani ni vizuri tukashirikiana lebo yangu na yake tukuze vipaji vingine kuliko mimi kwenda kuziba hiyo nafasi,” alisema Barnaba.

Barnaba anatarajia kuzindua albamu yake hiyo Agosti 16, 2022 jijini Dar huku Mtayarishaji Mkuu wa albamu hiyo akiwa ni Diamond Platnumz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live