Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Barnaba amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake wa muda mrefu anayefahamika kwa jina la Raya kutoka Tanga baada ya kukaa singo kwa miaka kadhaa tangu alipoachana na mkewe wa awali.
Jambo lililowashtua mashabiki wengi ni kwenye utambulisho huo Barnaba baada ya kutangaza kubadili dini na kufuata dini ya mwanamke ya Kiislamu ambapo kuanzi sasa Barnaba ni Muisilamu na atajulikana kwa jina la Mohammed ingawa yeye amesema atapenda zaidi aitwe (MO).
Penzi la Barnaba na Raya limekuwa na kashikashi kwa mda mrefu ambapo familia ya Raya ilikiwa haimkubali kabisa Barnaba huku kikwazo kikubwa kikidaiwa kuwa ni utofauti wa dini lakini baadaye waliyanaliza.