Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barnaba: Nimehawahi kushika sh bilioni 2

Barnaba M  Barnaba: Nimehawahi kushika sh bilioni 2

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva, Barnaba Classic, hivi karibuni kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kwamba amewahi kukamata kiasi cha Tsh bilioni 2 kwa mkupuo na kuwataka watu wasimchukulie poa.

Kwenye upande wa maoni, mashabiki wengi walionekana kumkataa kwa kusema kwamba hakuwa na hajawahi kuwa na uwezo wa kumiliki kiasi kikubwa cha pesa kama hicho kwa wakati mmoja.

Sasa Barnaba katika kipindi cha Refresh cha Wasafi, alifunguka wazi kwa kusema kwamba ukweli wake ndio huo na hana faida yoyote katika kusema uongo.

Alisema aliwahi pokea kiasi cha bilioni 2 kwa mara moja na pia kusisitiza kwamba alinukuliwa vibaya kwani kwa sasa hivi kuna uwezekano anapokea kiasi zaidi ya hicho.

“Watu wameninukuu vibaya, pesa ipi nimewahi kuishika kwa mkupuo, nikasema ni bilioni mbili. Ni kweli nimeshawahi kukamata bilioni mbili kwa mara moja lakini sasa hivi kuna uwezekano ninapata nyingi zaidi ya hizo,” Barnaba alilainisha mambo.

Barnaba alisema hajui ni kwa nini watu wanakaa kama vile hawamuamini katika maneno hayo na kuongeza kwamba pengine ni kutokana na hali yake ya kutoweka wazi kila kitu kwenye mitandao aghalabu.

“Mimi si mzungumzaji sana kwenye mitandao na lile lilikuwa ni swali niliulizwa na mtangazaji ni kasema ni bilioni mbili pap, lakini yaezekana sasa hivi ninazidi hapo.

“Nimekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu, mitikasi yangu ni mingi, sitegemei tu muziki, nina mirija mingi ya kupata hela. Kwangu bilioni mbili si kitu, mafanikio hayasemwi,” alisema Barnaba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live