Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraza laamuru muigizaji Robert DeNiro kumlipa mfanyakazi Bil. 30

Baraza Laamuru Muigizaji Robert DeNiro Kumlipa Mfanyakazi Bil. 30 Baraza laamuru muigizaji Robert DeNiro kumlipa mfanyakazi Bil. 30

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la waamuzi limeamua Kesi ya Muigizaji Robert DeNiro na aliyekuwa mfanyakazi wake binafsi Bi Graham Chase Robinson na kuamuru kuwa Mwanamama huyo kulipwa $12m (Tsh. Bilioni 30) katika kesi hiyo.

Bi Robinson alishitaki akidai kuwa alidhulumiwa na kufanyishwa kazi kama Mke wa Muigizaji huyo lakini Baraza halikumpata Muigizaji huyo ya madai bali kampuni yake ndio iliyowajibika.

Bi Robinson alikuwa kwenye orodha ya malipo ya DeNiro kwa miaka 11. Aliajiriwa kama msaidizi wake wa kibinafsi mnamo 2008, baadaye alipandishwa cheo na kuwa makamu wa rais wa uzalishaji na fedha katika kampuni hiyo.

Lakini baada ya kuacha Mwaka 2019 alishtaki kuwa alikuwa akinyanyasika kijinsia huku akipewa maneno makali ya kejeli, Walikanusha madai hayo.

Kampuni ya Canal Production ilimshtaki Mwana Mama huyo kwa matumizi mabaya ya fedha za ofisi, kuiba mali ya kampuni na kuhamisha zaidi ya $450,000 katika maili ya shirika la ndege kwenye akaunti yake ya kibinafsi lakini shtaka hilo lilitupiliwa mbali baada ya kukosekana na hatia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live