Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barakah The Prince amchana Kiba, amuita 'mganga wa kienyeji'

Baraka The Prince Kibaaaas.jpeg Barakah The Prince amchana Kiba, amuita 'mganga wa kienyeji'

Sun, 3 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Msanii wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amemtupia dongo msanii mwenzake, Alikiba ambaye wamewahi kufanya kazi pamoja chini ya Lebo ya Rock Star.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Barakah ameandika ujumbe huu; "MR Kero Nilikuwa mapumzikoni am Back now, sema nasikia kulikuwa na Sherehe za kuzaliwa kwa Mganga Moja wa kienyeji hapa nchini."

Ikumbukwe kuwa, Novemba 26, ilikuwa kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa msanii Alikiba na alionekana akisherehekea na wasanii wenzake pamoja na marafiki zake mbalimbali.

Barakah amekuwa akinukuliwa mara nyingi akisema Alikiba ni adui yake na hampendi, amekuwa akidai kuwa hamjui Kiba kama ni msanii wa Tanzania.

Cha kushangaza zaidi hivi karibuni alisusia mahojiano live na chombo kimoja cha habari nchini baada ya kuulizwa swali kuhusu Kiba, jambo hilo lilimfanya achukie, agome kujibu na kuanza kufoka kisha kuvua headphones na kuondoka ndani ya studio hizo huku akiwaacha watangazaji kwenye mshangao mzito.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live