Msanii wa Bongo Fleva, Baraka The Prince anadaiwa kufunga ndoa na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijawekwa hadharani.
Tetesi hizo zimeibuliwa na mbea wa mjini Soud Brown ambaye ameposti picha za mrembo huyo akiwa kwenye ghafla ambayo inahusishwa kuwa huwenda ndio ndoa yenyewe ambapo bibi harusi anaonekana akiwa amepaka hina.
Hata hivyo, Barakah mwwenyewe alipopigiwa simu kuhusu suala hilo aliruka vibaya na kusema hayupo Dar na hakuna ukweli wowote kuhusu suala hilo.
"Mimi nioe nyinyi waandishi msijue? Hapana bwana sijaoa mimi sipo Dar kwanza kama unasema sijui hiyo ndoa imefungiwa Magomeni," alisema Barakah.