Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraka The Prince arudi shule, amsifia kipa wa Yanga

Barakah Na Diara Baraka The Prince arudi shule, amsifia kipa wa Yanga

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: Mwananchi

Ukifanya kazi nzuri inavuta wengine kujifunza je, unataka kuamini hilo, hiki ndicho alichokisema msanii wa Bongofleva, Baraka the Prince, kuhusu kipa wa Yanga, Djigui Diarra anayemfurahisha jinsi anavyofanya kazi yake.

Msanii huyo ambaye ni shabiki wa Yanga, amesema Diarra akiwepo golini anakuwa na amani kuona timu inakuwa na ulinzi wa kutosha, hivyo kazi inabakia kwa washambuliaji kufunga.

"Diarra amekuja kuleta kitu tofauti, ambacho makipa wetu wazawa wanaweza wakajifunza kwa faida ya Taifa lao, anajiamini ana uwezo mzuri wa kutumia miguu, hivyo anawapunguzia kazi washambuliaji na kuwaongezea kujiamini,"amesema.

Kuhusu muziki Baraka amesema mwaka 2023 aliutumia kwa ajili ya kuandaa nyimbo za kutosha ambazo ataziachia mwaka huu.

"Nina nyimbo za kutosha, nilifanya hivyo kwa sababu mwaka huu (2024) narudi chuo kusoma Shahada ya Kwanza ya Uhandisi wa masuala ya simu (Tell Communication), kwani tayari nina Diploma nilioisoma 2013," amesema.

Mwimbaji huyo mwenye sauti nyororo na anayeimba nyimbo laini amebainisha kuwa anapenda nyimbo za Hiphop na baadhi ya wanamuziki anaowapenda ni kama Joh Makini, Fid Q na Nick Mbishi.

Chanzo: Mwananchi