Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baraka ‘Magufuli’ alivyotoboa kutoka kiwanda cha chai

52845 Pic+magu+feki

Wed, 17 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ili dhahabu ionekane mng’ao wake lazima iondolewe katika tope. Ndivyo kilivyokuwa kipaji cha mchekeshaji Baraka Mwakipesile maarufu Baraka Magufuli.

Kwa zaidi ya wiki mbili amekuwa gumzo mitandaoni baada ya kuigiza sauti ya Rais John Magufuli mbele yake.

Baraka alifanya hivyo Aprili 11, 2019 baada ya kuitwa na Rais Magufuli alipokuwa ziarani mjini Mafinga wilayani Mufindi, mkoani Iringa ambako msafara wake ulisimama kwa muda kusaliamia wananchi.

Tangu siku hiyo, Baraka amekuwa gumzo na video ya tukio hiyo ikisambaa kwa kasi katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Baraka anatoboa kuwa amekuwa akiigiza sauti ya Rais Magufuli tangu mwaka 2016, lakini kwa bahati mbaya huenda hakujulikana kwa sababu hakuwa akitumia majukwaa sahihi.

Akizungumza katika ofisi za Mwananchi leo Jumatano Aprili 17, 2019, Baraka amesema amechelewa kujulikana kwa sababu ya hali ya maisha hasa kwa kuwa muda mrefu amekuwa akikimbizana kufanya vibarua.

Amesema kabla ya umaarufu alikuwa akifanya kibarua katika kiwanda cha chai, jukumu lake likiwa ni kusaga majani.

“Nilipo hapa ni mwajiriwa na hata nilipokutana na Rais (Magufuli) niliombewa ruhusa ofisini kwa mkuu wangu wa kazi na uongozi wa halmashauri,” amesema.

Baraka amesema alianza kazi kiwandani hapo mwishoni mwa mwaka jana, kabla ya hapo alikuwa akisambaza maji kwa kutumia pikipiki kazi ambayo ilikuwa haimlipi.

“Pikipiki niliyokuwa naitumia ilikuwa ya kukodi, hivyo kwa siku  napata Sh7,000 mmiliki nampa Sh4,000, nabaki na Sh3,000 nikaona hailipi nikaamua kuomba kazi kiwandani hapo,” amesema.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz