Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Banana ni papa ndani ya bahari ya muziki

Sugu Banana 668434 Banana ni papa ndani ya bahari ya muziki

Sat, 25 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unakuwa kama unatazama documentary ya Wild Indian Ocean. Unamwona samaki mkubwa anatamba baharini, anachezea maji atakavyo. Samaki wadogo wanapisha mbali.

Banana Zorro kwenye muziki ni sawa na samaki mkubwa baharini. Kiapo changu ni performance yake kwenye Bongo Flava Honors, Alliance Francaise, Novemba 24, 2023.

Banana knows fashions. Ametinga Steroid Boots nyeusi, shingo fupi. Outfit inakuja kama panjabi inakataa. Nyeusi. Inameremeta. Kichwani durag black. Machoni sunglass sport yenye frame black and white. Shingoni hadi mkono wa kushoto, kachakaa madini meupe. Mkono wa kulia kavaa saa black.

Huo ndio mtupio wa Banana, katika sherehe maalum ya kutambua mchango wake wenye thamani kubwa kwenye muziki wa Bongo Flava.

Host wa event, mtunukiwa wa Challenge Coin ya Department of State, USA, Sugu The Jongwe, ameshasoma induction speech kwa ajili ya Banana, kisha anaua na ngoma “Chini ya 18”. Anaita kutest mitambo.

Sugu anamwita Banana jukwaani. Anamkabidhi plaque ya heshima. Kilichofuata baada ya hapo ni uchawi wa binadamu aliyejaliwa karama ya kushangaza.

Wimbo “Big Boss” anauchezea, unakuwa intro ya show. Kisha, audience inapagawa kwa sauti ya juu “Mama Kumbena” inacharazwa. Banana mhuni sana, Mama Kumbena anaicheza kwa versions kama tatu. Juu, chini kisha akaipeleka kwenye mduara.

“Nataka Kuwa Nawe” hiyo hapo. Watu wanacheza. Banana anawachezesha. “Niko Radhi”, inaimbwa na kila mtu. “Segnora” iliihamisha hadhira hadi Spain na Latin yote.

Tazama mpangilio wa nyimbo. “Sio Kama Wale” hadi “Pressure”. Halafu “Bado Kidogo”, “Mapenzi Gani”, “Pole Rafiki”, “Wasiwasi”, “Natamani”, “Anakudanganya”, “Nzela”, “Sogea Nikushike Mkono”, “Mama Yangu”, halafu “Zoba”.

Banana ni musical prodigy. Aliua kila pembe ya event. Anacheza na sauti yake ni imara. Nishati aliyoanza nayo ndio alimalizia. No wonder Banana ndiye mwanamuziki mwenye tuzo nyingi zaidi za Best Male Vocalist kutoka Kili Music Awards.

Unataka comment yangu? Banana is something to write home about. Yeye katika muziki, ni kama papa baharini. Anatisha ile mbaya.

Ex-Mayor wa Ubungo na Kino, Boni Jacob akaninong'oneza: "Banana ni maestro wa muziki."

Ndimi Luqman MALOTO

Chanzo: www.tanzaniaweb.live