Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Banana Zorro 'The Bongo Flava Tanzania'

Banana Zorro Rew Banana Zorro 'The Bongo Flava Tanzania'

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nasikiliza masterpiece “Siwezi Sema” wa Deo Mwanambilimbi. Kazi ina miaka kibao, ila haichuji kwa sababu Banana Zorro crafted the song.

Mawazoni inanijia ngoma “Umebadilika”. Ni lifetime hit kutoka kwa Killer Msodoki. Banana is everything in the song. Intro inakuhakikishia wimbo ni mzuri. Chorus, Banana ameua. Ubeti wa tatu ni bonge la hook.

Track record ya Banana, inathibitisha kuwa kila anapo-install sauti yake kwenye wimbo, hugeuka dude tamu ajabu. Shaba inakuwa dhahabu. Kama ni dhahabu, hupanda thamani hadi tanzanite.

Kula chuma “Basi Aje” cha Deputy Minister “MwanaFA”. Burudika na sauti ya Banana ndani yake. Workmanship of Banana ni top cream, siku zote.

Naitafakari safari ya kimapinduzi kuivusha Bongo Flava kutoka utamaduni mamboleo. Harakati mithili ya counterculture, halafu underground. Leo hii Bongo Flava ni tasnia. Yapo majina yenye hadhi ya almasi, tanzanite dhahabu hadi shaba.

Mchango wa mtu ndio kipimo cha nyota begani. Banana, tangu yule mvulana wa B Love M akiwa na partner wake Masiga hadi Banana “big man” akimiliki B Band, bila shaka jina lake lina-score alama za juu katika madaraja ya wale walioifanya Bongo Flava kuwa industry.

Banana is our own Bongo Flava tanzanite. File lake la huduma limesheheni pini back to back kwa miongo zaidi ya miwili ya utumishi. Sauti yake pia imehusika kufanya kazi za wanamuziki wengine wengi kuwa bora.

Project kwa project. Story ya dada aliyekata ringi nyumbani “Nzela”, hadi visa vya mama mkwe “Mama Kumbena”. Ule “Wasiwasi” wake ukamgeuza “Zoba”. Unaweza kuunda jukebox inayovutia mno kupitia nyimbo za Banana.

Tangu akiwa mvulana akipambana safarini kuwa mwanaume, Banana alijitengeneza kitaasisi, akaajiri na kugawana jasho la sanaa na vijana wenzake wenye vipaji kupitia B Band.

Ukuu huo wa Banana, bila shaka ndio umeishawishi Bongo Flava Honors Academy, kuitenga Novemba 24, 2023, kuwa siku maalum kwa ajili ya Banana.

Siku hiyo, Banana atasimikwa hadhi ya Bongo Flava Honors. Atatunukiwa plaque maalum. Ataperform kwa live band, nyimbo zake zote. Sugu The Jongwe, ataongoza dhifa ya kumpa maua Banana.

Kiwanja ni Alliance Francaise, Upanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live