Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bahati kutoka kivingine na Aslay (+video)

Mon, 12 Feb 2018 Chanzo: bongo5.com

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Bahati amefunguka ujio wa kolabo nyingine na msanii kutoka Bongo baada ya kufanya vizuri na ngoma ‘Nikumbushe’ ambayo alimshirikisha Rayvanny.



Muimbaji huyo amesema kwa mwaka huu anatarajia kusikika katika ngoma moja na Aslay ambayo ameshirikishwa na tayari kila kitu kwa sasa kimekamilika.

“Tanzania nina kolabo kadhaa ambazo zinakuja na ninashukuru Watanzania walinipokea vizuri na wimbo wangu wa Nikumbushe niliomshirikisha Rayvanny kutoka Wasafi.”  amesema.

“Huu mwaka tayari nina ngoma kubwa sana, kolabo kubwa sana na Aslay pia tuna video kubwa sana ambayo tuli-shoot Zanzibar ipo tayari ni wimbo wa Aslay ambao amenishirikisha, kwa hiyo ni wimbo ambao atautoa kwa muda wake.” Bahati ameiambia Bongo5.

Chanzo: bongo5.com