Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bahati ahofia kufumaniwa na mkewe

Bahati Ahofia Kufumaniwa Na Mkewe.png Bahati ahofia kufumaniwa na mkewe

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: Radio Jambo

Msanii wa kizazi kipya nchini Bahati Kioko amefichua kwamba hofu yake kubwa katika maisha ni mke wake Diana Marua kumfumania akiwa kitandani na mwanamke mwingine.

Bahati alifichua haya katika mchezo wa chemshabongo ambao walikuwa wanafanya na mke wake Diana kupitia chaneli yake ya YouTube.

Wanandoa hao walishiriki mchezo wa ‘Truth or Dare’ ambapo swali la kwanza lilikuwa la Diana kwa mumewe.

Diana alimuuliza Bahati hofu yake kubwa kuhusu kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na yeye, hata baada ya kumzalia watoto watatu.

“Hofu yangu kubwa ni… unajua vile wewe uko na hasira kama za Mkisii, naogopa siku moja unifumanie nikishiriki mapenzi na mwanamke mwingine… simaanishi kwamba siku moja nina wazo la kukusaliti kimapenzi, ni hofu tu na nimefanya kujibu swali lako,” Bahati alijitetea mbele ya mke wake aliyeonekana kupandwa na mori kwa jibu hilo ambalo kwa dalili zote hakulitarajiwa kutoka kwa mume wake kipenzi.

Bahati alisema kwamba hofu yake kubwa ni kwamba mke wake akimfumania akichepuka atamuua na kumsafirisha jongomeo, kitu ambacho Marua alikiri kwamba ndicho kitu pekee ambacho kitakuwa katika mawazo yake muda huo pindi tu atakapomfumania.

Diana alizidi mbele kumuuliza Bahati ni lini anatarajia kufanya hivyo ili naye afanye mipango ya kumfumania na kumfanyia alichokiri.

“Wakati mwanamume ameamua kuongea, inakuambia kile ambacho kiko ndani ya moyo wake. Fanya kitu unachotaka kufanya,” Diana alimwambia Bahati.

Chanzo: Radio Jambo