Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu tale asimulia alivyouza mihogo kabla kushika pesa

Babu Tale Big Babu tale asimulia alivyouza mihogo kabla kushika pesa

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kusini Mashariki, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ amesimulia sehemu ya msoto aliowahi kuupitia kabla haashika hela ambapo alisema aliwahi kuwa muuza mihogo.

Babu Tale ametoa sehemu hiyo ya historia yake alipokuwa kwenye kipindi cha Big Sunday Live kinachorushwa na Wasafi TV ambapo alieleza ishu hiyo ilimtokea wakati anasaka mlango wa kutokea kimaisha.

“Wakati huo kuna mtu alishauri niuze mihogo, nikawa natoka mihogo mkoa naleta Kariakoo nikiwa mwenyewe kwenye kenta.

“Nakumbuka wakati huo nilikuwa sijamuoa marehemu mke wangu, nikawa natenga mihogo kidogo nakwenda kumuhonga mke wangu,” alisema Tale.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live