Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu Tale atunukiwa Stashahada ya Udaktari wa Heshima

Babu Tale Atunukiwa Stashahada Ya Udaktari Wa Heshima Babu Tale atunukiwa Stashahada ya Udaktari wa Heshima

Fri, 27 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambaye pia ni Meneja kwenye Record Label ya WCB, Hamisi Taletale 'Babutale' leo Januari 27, 2023 ametunukiwa stashahada ya udaktari wa heshima.

Babu Tale ametunikiwa stashahada hiyo kutokea Taasisi ya 'Academy of Universal Global Peace' (AUGP-USA) ya nchini Marekani.

Baada ya kutunukiwa Babutale amezungumza yafuatayo;

“Nashukuru sana kwa nafasi hii niliyopewa, hii ni kwa sababu ya yale niliyoyafanya kwenye kazi zangu za siku zote, leo hii mimi ni Artist Manager lakini vilevile ni Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, yote haya nimeyafanya kwa wakati mmoja wakaona si mbaya wanitunukie.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live