Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu Tale amvulia kofia Isarito

Babu Tale Amvulia Kofia Isarito Babu Tale amvulia kofia Isarito

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na Meneja wa #Diamondplatnumz @babutale amemvulia Kofia Muigizaji @isarito_tmt kutokana na uwezo wake wa kuigiza . Babu Tale amempongeza Isarito kupitia ikurasa wake wa Instagram kwa kuandika ujumbe huu chini

"Leo nimechuma maua yenye Oksijeni ya pongezi nyingi Juu ya Kijana Mwenye juhudi ziliandikwa kwa mpango wa jasho.

Acha leo nimpe mauwa yake huyu mwamba japokuwa mimi sijawahi kumuona uso kwa uso, ila nimejikuta tu nakuwa Shabiki yake kwa kile anachokifanya kwenye kila kazi yake yake ya Sinema.

Ndugu yangu @isarito_tmt najua unajua kuwa Mimi sikujui hata chembe, lakini nataka ufahamu kuwa, Mimi ni Shabiki yako namba moja kwa sasa. Naomba upige kifua chako na jue kuwa, Wewe ni Mkali haswaa na nakuona mbali sana katika safari ya heshima na mafanikio.

Kikubwa endelea kusimamia kile ambacho Mungu amekupa kwani naamini lazima kitatoa matunda kwako, familia yako na Nchi kwa ujumla. Endelea kukaza kwakuwa jasho la haki ya kazi yako litakulipa thamani ya heshima itakayoishi vizazi na vizazi"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live