Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu Tale ampa maua yake Dully Sykes

Dully Sykes 782 892 800x600 Babu Tale ampa maua yake Dully Sykes

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Diamond Platnumz na WCB Wasafi kwa ujumla, Babu Tale amempa maua yake Dully Sykes kutokana na mchango wake ndani ya Bongofleva.

Babu Tale ambaye pia Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, kupitia Instagram ameandika ujumbe mrefu kumuhusu Dully Sykes.

Chini kile alichoandika Tale. Muziki huwa unawachagua watu, japokuwa watu wengi huchagua muziki. Katika kulinda ukuaji wa tasnia hii muziki wenyewe huwa unaongea na kutoa utambulisho wa watu wake.

Leo ninayofuraha kuwakumbusha kuwa muziki wa nchi hii umemchagua Prince Dully Sykes kuwa kiungo kilichoibua na kukoleza ladha ya muziki wa kizazi kipya (Bongofleva).

Wakati huu ambapo muziki wa Bongofleva umekamata usukani ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, natamani Jamii yetu ijue uhusika wake wa moja kwa moja katika uwepo wa Bongofleva tunayoiona leo kwa namna alivyotoa jasho na maarifa katika kuasisi na kuukuza muziki huu.

Sisi familia ya Bongofleva tunakushukuru na kuutambua mchango wake na yeye ni Legend wa muda wote na jezi yake haipaswi kuvaliwa na mtu mwingine bali itastaafishwa kwa heshima.

Utakumbuka hadi sasa Dully Sykes ametoa albamu tatu, Historia ya Kweli (2003), Handsome (2004), Hunifahamu (2005) na anatajwa kama miongoni mwa waanzilishi wa Bongofleva.

Wimbo wa Dully Sykes ‘Julieta’ ndio wimbo wa kwanza wa Bongofleva wa kuimba, kwani awali muziki uliokuwa ukifanyika ni wa Rap zaidi ingawa Dully naye mwanzo alifanya Rap.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live