Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu Tale afunguka ukaribu wa Harmonize na Sallam SK

Sallam Harmonize Babu Tale afunguka ukaribu wa Harmonize na Sallam SK

Sun, 18 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki na Meneja wa Msanii @diamondplatnumz Hamisi Tale Tale @babutale ameweka wazi kuwa anafurahishwa na ukaribu wa meneja mwenzake @sallam_sk na CEO wa Lebo ya @kondegang ambaye aliwahi kuwa msanii wa WCB, @harmonize_tz.

"Tatizo Watanzania wanapenda sana vita hamna kitu kiliniuma kama Harmonize na Sallam kutokusalimiana (kupeana mikono) kwenye msiba wa marehemu mke wangu iliniuma sana.

"Ile ilikuwa sherehe ya mwisho ya mke wangu, lakini nilivyoona juzi wanasalimiana kwa kukumbatiana kiukweli nilifurahi sana maana yake hawana Tatizo, mimi nisikuongopee hizi dhana za Sallam SK kwenda Konde Gang sio za kweli," amesema @babutale.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live