Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu Tale: Tutapunguza asilimia za kugawana na wasanii wanaokuja WCB

Babu Tale Big Babu Tale: Tutapunguza asilimia za kugawana na wasanii wanaokuja WCB

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Wasafi Classic Baby (WCB), Hamis Tale amesema kwa wasanii wanaokuja kujiunga na lebo hiyo kwa sasa, watakutana na panga la mikataba ya asilimia 30 badala ya 40 waliyokuwa wanatoa awali.

Babu Tale ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa anazungumza na Wasafi TV kwenye kipindi cha Big Sunday Live ambapo alieleza kuwa, kutokana na muziki ni bishara na msanii anapofika kuna uwekezaji unafanyika hivyo lazima wafuate utaratibu huo.

“Wewe kama Beyonce anachukua asilimia 30 kwa nini na sisi tusiende huko? Hii ni biashara sio kwamba tunamsaidia mtu, tunafanya biashara,” alisema Tale.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live