Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu Tale: Mungu ananiandalia mke mzuri

TALE NA WANAWE Babu Tale: Mungu ananiandalia mke mzuri

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Jimbo la Kusini-Mashariki mkoani Morogoro, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ amesema ana imani, Mungu atampa mke mwingine mzuri baada ya kufiwa na mkewe miezi kadhaa iliyopita.

Babu Tale amesema, baada ya kufiwa na mkewe, alipata msiba mwingine wa kuondokewa na mama wa mmoja wa watoto wake ambaye watu wengi walikuwa hawamfahamu.

Kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wake wa Instagram, Tale ameposti picha inayonesha watoto wake wane na kusindikiza na ujumbe huu:

"Najua wengi wenu mtajiuliza huyu mwengine ni nani..? Sababu hao watatu sura zao sio ngeni sana machoni mwenu..huyo mgeni kwenu anaitwa ZAHID.. nimwanangu pia.. kama ilivyo hao watatu.

“Huyu nae nimempoteza mamayake miezi miwili iliyopita…sina budi kumshukuru Mungu kwa kila Mtihani anaonipa..kwa maana anaamini nitauweza... siwezi tena kulia, zaidi nakuomba uendelee kunifungulia riziki kila uchwao..na naamini unaniandalia Mama yao mpya (mke mzuri) wakuja kuwalea nakuwaongoza Kwenye misingi mizuri yakumjua Mungu...”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live