Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu Tale: Marehemu mke wangu ndiye alinifanya niache uchekeshaji

Babu Tale Na Mkewee Babu Tale: Marehemu mke wangu ndiye alinifanya niache uchekeshaji

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hamis Taletale ambaye ni mbunge wa Kusini Mashariki amesema, zamani wakati anahaso kutoka kimaisha, alikuwa mchekeshaji ambapo alikuwa mkali wa kuigiza sauti za viongozi lakini marehemu mkewe ndiye alimshauri aache na kweli akatii.

Babu Tale ameyasema hayo juzikati alipokuwa akifanya mahojiano na Wasafi TV ambapo alitumia kipindi cha Big Sunday Live kusimulia mambo mbalimbali aliyowahi kuyapitia maishani alipokuwa anahaso aweze kuisaidia familia yake kwani alitokea kwenye familia masikini.

“Nimefanya kazi nyingi sana na sijawahi kufeli. Nilikuwa naigiza sauti zaidi ya hawa kina MC Babu Ayubu lakini nililazimika kuacha baada ya marehemu mke wangu kuniambia niache.

“Aliniambia niache na mimi nikiangalia mke wangu kifaa sasa nijifanye nakataa halafu nikose mtoto inaingia akilini kweli?” alihoji Babu Tale.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live