Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba wa Ommy Dimpoz afunguka kuhusu kazi yake ya Bajaji

Baba Mzazi Wa Ommy Dimpoz Baba wa Ommy Dimpoz afunguka kuhusu kazi yake ya Bajaji

Wed, 14 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kupitia kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV, Baba mzazi wa supastaa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz', aitwaye Mzee Faraj Nyembo amefunguka kuhusiana na kazi yake ya uendeshaji Bajaji huko Mjini Sumbawanga, akidai anashukuru anapata riziki kubwa ukilinganisha na kazi yake ya malori aliyokuwa akiifanya kabla.

"Maisha ya hapa Sumbawanga mazuri, baridi, chakula cha kutosha. Kazi yangu ni dereva wa magari makubwa lakini niliona Kwa sasa nipumzike maana nilikuwa nimeacha familia muda mrefu.

"Nimekaa Malawi, Zambia miaka miwili nimeamua nirudi nikae na familia. Nimenunua bajaji zangu mbili nimeamua nifanye shughuli zangu za bajaj kwa sababu zote ni usafirishaji tu.

"Kwa siku kwenye bajaj hapa Sumbawanga naweza kupata hadi Tshs Elfu 40 hadi 50 inategemea na hali ya usafiri. Maana muda mwingi nakuwa kwenye ibada,” amesema baba Dimpoz.

Mzee Nyembo amedai Kipato anacho kipata kupitia Bajaji kwakuwa anaendesha mwenyewe kina kidhi mahitaji yake na familia yake ukilinganisha na kazi ya malori aliyokuwa akisubiri kwa muda mrefu ujira wa laki mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live