Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba wa Beyonce alaumu ubaguzi wa rangi kwa mwanae

Matthew Knowles Beyonce Today Main 191002 Baba wa Beyonce alaumu ubaguzi wa rangi kwa mwanae

Tue, 10 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mathew Knowles, Baba mzazi wa mwanamuziki nyota wa muziki wa pop duniani, Beyoncé, amekuja juu baada ya jina la binti yake kutokuwepo kwenye list ya wasanii watakaowania Tuzo za Muziki wa Country za mwaka huu.

Majina ya watakaowania tuzo hizo yalitangazwa hivi majuzi, huku jina la Beyoncé likikosekana licha ya kuwa na wimbo nambari moja wa muziki wa 'Country' pamoja na albam iliyotoka mwezi March mwaka huu.

Mzee Mathew Knowles aliwashutumu waandaaji wa tuzo hizo akiwaita wabaguzi wa rangi kwa kuwa hawaangalii uwezo na mafanikio ya mtu bali rangi.

Albamu ya Beyoncé ‘Cowboy Carter’ ndiyo albamu mpya ya 'Country' iliyopewa sifa kedekede na ambayo imeuza zaidi mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live