Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Baba wa Angelina Jolie asikitishwa na bintiye kuhusu Gaza

Angelina Jolie Rd Anusurika kufa baada ya kung'atwa na mamba

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji Mkongwe na mshindi wa tuzo za Oscar Jon Voight (84), ambaye ni baba mzazi wa Muigizaji Angelina Jolie ameeleza kusikitishwa kwake na maoni ya binti yake kuhusu mashambulio ya Israel yanayoendelea huko Gaza.

Kupitia mtandao wa Instagram Jolie (48), aliposti ujumbe uliosema kuwa ”shambulio la kigaidi la Hamas haliwezi kuhalalisha kulipuliwa na kupoteza maisha ya watu wasio na hatia huko Gaza, ambao hawana pa kwenda, hawana chakula au maji,hakuna uwezekano wa kuhama na hata haki za msingi za binadamu za kuvuka mpaka kutafuta hifadhi.

Mashambulio ya mabomu yanasababisha mahitaji mapya ya kibinadamu kila siku. Kunyimwa misaada, mafuta na maji kwa pamoja ni kuwaadhibu watu, ubinadamu unataka kusitishwa kwa mapigano mara moja”.

Katika video iliyopostiwa mitandaoni, iliyoambatana na kichwa cha habari ” Ukweli na Uongo” akiwa amekaa mbele ya bendera ya Marekani, mzee huyo amesema ”nimesikitishwa sana na binti yangu, kama walivyo wengi, binti yangu hana ufahamu wa heshima ya Mungu wala kweli ya Mungu”.

”Hili ni suala la kuharibu historia ya nchi ya Mungu, nchi takatifu, nchi ya wayahudi. Hii ni haki kwa wana wa Mungu wa nchi takatifu”

”Jeshi la Israeli ni lazima lilinde udongo wake, watu wake. Hii ni vita, haitakwenda kuwa kama upande wa pili wanavyotaka, haiwezi kuwa ya kistaarabu sasa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live