Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Baba aiweka sokoni Pete ya Kobe Bryant kwa milioni 358

Kobe Ring Baba aiweka sokoni Pete ya Kobe Bryant kwa milioni 358

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Joe "Jellybean" Bryant, Baba mzazi wa aliyekuwa nyota wa mpira wa kikapu marehemu Kobe Bryant, ameiweka kwenye mnada kwa dola $141,000 (sawa na sh milioni 358 za kibongo) pete ya Kobe Bryant ya ubingwa wa NBA mwaka 2000 alioupata akiwa na timu yake ya Lakers.

Pete hiyo iliyowekwa sokoni na Mzee Bryant ina karat 14 za dhahabu, pamoja na vipande 40 vidogo vya almamsi huku ikiwa na maandishi yaliyoandikwa 'LAKERS'. 'WORLD CHAMPIONS', "BRYANT" pamoja na namba yake ya jezi '8'.

Hata hivyo pamoja ya kwamba pete hii ina dhahabu pamoja na almasi, lakini sio yenyewe halisi kwani Kobe wakati wa uhai wake alitengeneza hii kama nakala maalum kwa ajili ya zawadi kwa baba yake na akaitunza ile original kwa ajili yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live