Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo ni mbuzi kama mbuzi wengine, ana matatizo ya akili-Mlela

Mlela Na Baba Levo Baba Levo ni mbuzi kama mbuzi wengine, ana matatizo ya akili-Mlela

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka kwenye kiwanda cha filamu Bongo, Yusuf Mlela ameamua kumtolea uvivu Fundi Majumba, Baba Levo kwa kumuambia yeye ni mbuzi kama walivyo mbuzi wengine.

Mlela ameibuka kumjibu Baba Levo ambaye juzikati aliibua tafran baada ya kuwasema wasanii wa Bongo Muvi hawajitambui na kwamba hawana kitu mifukoni mwao.

“Baba Levo ni mbuzi tu kama mbuzi wengine tunamnywa supu, nilimdharau tangu nilipomsikia anasema angekuwa mwanamke angemzalia mwanaume, kama mwanaume hauwezi kutamanani kumzalia mwanaume mwenzako, ana tatizo la afya ya akili,” alisema Mlela.

Mlela alisema kama Baba Levo ataona namna gani basi amuambie tu wakutane ulingoni amtandike za chembe biashara iishe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live