Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo na Tetema ya Rayvanny kufutwa “S2Kizzy anataka hela zake”

TETEMA RAYVANNY S2KIZZY Baba Levo na Tetema ya Rayvanny kufutwa “S2Kizzy anataka hela zake”

Sat, 13 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa Bongo Fleva ambaye pia ni Official Chawa wa Diamond Platnumz, Baba Levo amefunguka kuhusu kitendo cha video ya ‘Tetema’ ya msanii Rayvanny aliyomshirikisha Diamond kufutwa katika mtandao wa YouTube.

Video hiyo inadaiwa kufitwa na proiducer wa wimbo huo, Salmin Kassim maarufu kama ‘S2Kizzy’ kwa madai kwamba anamdai pesa rayvanny ambazo hajamlipa, hivyo ameshakanusha kuhusika na kitendo cha kufuta video hiyo.

Akihojiwa na moja ya chombo cha habari, Baba Levo amesema kuwa S2Kizzy anataka hela zake, kwa hiyo rayvanny hana budi kumlipa ili awe huru na video yake irudishwe hewani.

“Kwa sasa S2Kizzy na Rayvanny ni watu wanaofanya kazi pamoja, naona sasa hivi kila mtu anataka hela zake. Kama S2Kizzy ameamua kufanya hayo ili apewe hela zake hiyo ni yeye mwenyewe.

“Ujumbe ninaoweza kumpa S2Kizzy ni kwamba, hapaswi kumshambulia Diamond kwa aina yoyote kwa sababu alikuwa mdogo sana, lakini kupitia Mondi amemfanya Kizzy kuwa mkubwa sana.

“Kwa sababu hajasaini mkataba wa kufanya kazi na WCB, anaweza kufanya kazi na watu wengine akapata pesa. Atumie nguvu yake kama mtaji wa kupata pesa. Ukimsikia anadai pesa ni haya haya matatizo.

“S2Kizzy anapaswa kumshukuru Diamond vibaya mno, akimaliza kumshukuru baba yake na mama yake, anayetakiwa kufuata kumshukuru ni Diamond,” amesema Baba Levo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live