Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo awatahatharisha Nuh Mziwanda na Nedy Music kuhusu Shilole, ‘Mtagongwa makofi’

1474 Shilole 212313 TZW

Thu, 18 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Baada ya Shilole kufunga ndoa na mpenzi wake Uchebe, msanii Baba Levo amewataka Nuh Mziwanda na Nedy Music kukaa mbali na Shilole.



Nuh Mziwanda na Nedy Music waliwahi kutajwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Shilole kipindi cha nyuma.

Baba Levo amesema wasanii hao wasijewakatumia hicho kama kigezo cha kuendelea kwa karibu na Shilole kwani sasa ni mke wa mtu na endapo watafanya hivyo wataambulia makofi kutoka kwa uchebe.

“Hiki kilichotokea sasa hivi naomba Nuh Mziwanda Nedy Music sasa watulie Uchebe amekomaa atakupiga kofi, mtagongwa makofi biashara itaisha,” amesema.

“Na kuanzia sasa hivi Shilole atulie amuheshimu mume wake ambaye amekubaliana naye kuendesha maisha,” amesisitiza.

Usiku wa January 14 mwaka huu ndipo ilifanyika sherehe ya ndoa ya Shilole na Uchebe ambapo Baba Levo alikuwa MC wa shughuli hiyo.

Chanzo: bongo5.com