Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo atimiziwa jambo lake na Serikali

BABA LEVO Baba Levo atimiziwa jambo lake na Serikali

Thu, 18 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii na Diwani wa Mwanga Kigoma Mjini Baba Levo ametimiziwa ombi lake kwa Serikali la kutaka shughuli za kisanaa ziendelee ili wasanii wapate pesa kwa sababu taarifa ya ongezeko la ugonjwa wa Corona kupungua.

Sasa jambo lake hilo limetimia baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutangaza shughuli hizo ziendelee wakati anavunja Bunge la 11 Jijini Dodoma.

Akizungumza kwenye Show ya eNewz Baba Levo alisema "Naomba Serikali na viongozi wa Serikali wanisikilize, kama umeruhusu wananchi waendelee kufanya biashara zao halafu watoto ukawarudisha nyumbani wasisome sasa hao wazazi si watuchukua Corona na kuupeleka nyumbani, sasa si bora shughuli zingine zifunguliwe tutafute pesa na vurugu ziendelee"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live