Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo ataka Diamond ajengewe sanamu

Baba Levo Na Diamond Baba Levo ataka Diamond ajengewe sanamu

Tue, 31 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya wimbo wa Diamond Platnumz 'Yatapita' kushika nafasi ya 3 kwenye mtandao wa Shazam yani wimbo unaotafutwa zaidi dunia kupitia mtandao huo ikiwa ni siku 9 tangu wimbo huo uachiwe rasmi, sasa Baba Levo anashauri Diamond ajengewe sanamu kwa makubwa aliyoyafanya kwenye muziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Baba Levo amepost orodha inayoonyesha wimbo huo unashika nafasi ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki na Sudani Kusini huku ukishika namba 3 duniani kwa kutafutwa zaidi na kuandika;

"Viongozi wanaohusika na SANAA YETU Hawapaswi Kuona Aibu KUMPA @diamondplatnumz KITU KITAKACHO KUMBUKWA NA VIZAZI VIJAVYO ...!! NASHAURI LIWEKWE SANAMU LAKE MAHALA...!!AMEFANYA KAZI KUBWA SANA KUITANGAZA HII NCHI....!!'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live