Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo ataja sababu za kutomlipa P Funk pesa zake

Baba Levo Pua Baba Levo

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni Chawa wa Diamond Platnumz amefunguka sababu za kutomlipa producer mkongwe wa Bongo, P Funk Majani akidai kuwa wimbo huo ulikuwa maalum kwa ajili ya kumtetea.

Akifanyiwa mahojiano hivi karibuni, Baba Levo amekanusha alichokisema P Funk kuwa alimdhulumu pesa zake miaka 15 iliyopita.

“Diamond anaongoza kwa kuwafanya wasanii kuwa wakubwa, Rayvanny ametakiwa kulipa tsh milioni 800 ili aondoke, amelipa, Harmonize amelipa Tsh milioni 500, niambie msanii wa P Funk anayeweza kuwa na hiyo pesa?

“Mimi nimetoka Kigoma nikaja kwa P Funk kurekodi, nimelipa pesa zangu nikafanya kazi na kazi nyingine bado hazijatoka mpaka leo, ni miaka mingi 2004. Hakuna kitu chochote kibaya nilichomfanyia wala sijawahi kumdhulumu kama anavyosema.

“Wimbo anaosema ni Wanye ambao niliimba wakati huo alikuwa akitukanwa na Nay wa Mitego, nikatoa wimbo kumtetea Majani, nikamnyea Nay, sasa nikutetee halafu nikulipe tena? Uliona wapi?" amesema Baba Levo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live