Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo amchana Nandy

Nandy Safi Baba Levo amchana Nandy

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chawa wa Diamond na msanii wa Bongo Fleva, Baba Levo amemchana kiaina Nandy kwamba alimwambia asirukeruke kwani madhara yake ni kuvimba miguu.

Kipande ambacho kimevuja kwenye kurasa mbalimbali za Instagram kimemuonesha Billnass akilazimika kumkandakanda Nany miguu iliyovimba baada ya kufanya shoo yake hivi karibuni mjini Songea.

“Wakati tunasema Nandy asirukeruke alikuwa hasikii sasa kilichomtokea ndio hiki,” alisikika Baba Levo kwenye klipu hiyo ya video inayomuonesha Nandy akiwa amekaa kwenye kochi na Billnass akimkandakanda miguu.

Kwenye mahojiano ya hivi karibuni, Nandy alieleza kuwa, ameshaelezwa na daktari kuwa licha ya kuwa mjamzito, anaweza kufanya shoo hivyo yupo salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live