Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo adai kushushiwa kipigo na Harmonize

Levo Harmonizeee Baba Levo adai kushushiwa kipigo na Harmonize

Mon, 12 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Asubuhi ya jana Mwanamuziki/Mtangazaji Baba Levo kupitia ukurasa wake wa Instagram ametoa taarifa kwamba usiku wa kuamkia jana ameshambuliwa na mwanamuziki Harmonize.

Watu wengi hawakuamini maneno ya Baba Levo maana wamezoea mara nyingi kumuona akimtania Harmonize kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa chanzo ambacho hakijataka kutajwa jina lake kimeelezea, “Usiku wa Kuamkia leo Harmonize na Baba Levo walikuwa kwenye Casino moja Jijini Dar es Salaam.

Harmonize kwenye kamari alipoteza milioni kumi na Baba Levo baada ya kugundua akanza kumcheka na kumtania.

Harmonize aliyekuwa na hasira za kupoteza pesa alimpiga kofi Baba Levo, Baba Levo akiwa bado anaongea alijing'ata mdomoni, damu zikaanza kutoka".

Baada ya Mkasa wa Kupigwa Kofi na Harmonize, Baba Levo Masaa kadhaa yaliyopita ame-post "RB" ya Polisi akimaanisha kuwa tayari amemshitaki Harmonize lakini ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa hii ndio mara ya mwisho kumshitaki mtu, endapo mtu atataka ugomvi nae basi hawezi kukaa kizembe kama alivyofanya kwa Harmonize bali watapigana ipasavyo na kesi haitapelekwa polisi.

Kwa upande wa Harmonize bado hajafunguka lolote kuhusiana na Sakata hili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live