Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo adai kumkonektia wanaume Shilole

BABA Baba Levo adai kumkonektia wanaume Shilole

Mon, 15 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii na Diwani wa Mwanga Kaskazini kupitia chama cha ACT Wazalendo Manispaa ya Kigoma Ujiji, Baba Levo amefunguka ukaribu wake na msanii Shilole ambao umedumu kwa muda wa miaka 12 au 13.

Akizungumzia ukaribu wake na Shilole , Baba Levo amesema Shilole alikuwa mwanamke mzuri na aliamini akiwa naye karibu atavutia japo wakati wanaanza urafiki wao alimpenda ukweli kutoka moyoni.

"Mimi na Shilole tuna miaka zaidi ya 12 au 13, alikuwa mwanamke mzuri halafu nilikuwa sina pesa ila niliamini nikiwa naye karibu nitanukia, mwanzo nilikuwa nampenda kutoka moyoni, na mahusiano yake mengi mimi ndiyo nimemkonektia kwa wanaume kuanzia Nuh Mziwanda, Nedy Music na wengineo, pia nilikuwa nampa ushauri" amesema Baba Levo

"Shilole anapenda sana na akishapenda sehemu yeye ni wivu tu, ugomvi, mkorofi na anapenda sana kutawala, kwa hiyo unajikuta unaanza kuamua kesi baada ya kesi, kwa mfano kesi za Nuh na Shilole nimeshaziamua zaidi ya mara 56" ameongeza

Chanzo: www.tanzaniaweb.live