Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo aanika sababu za Rayvanny kuondoka WCB “Aitaja management”

Levo Baba Levo aanika sababu za Rayvanny kuondoka WCB “Aitaja management”

Fri, 22 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni Chawa wa Diamond Platnumz, Baba Levo amefunguka sababu za msanii Rayvanny kama mshikaji wake kuondoka katika Lebo ya WCB akidai kuwa alitaka awe huru kufanya mambo yake.

Baba Levo amesema hayo ikiwa ni wiki chache baada ya Rayvanny kutangaza kuachana na Lebo na hiyo aliyoitumikia kwa miaka sita na kwenda kusimamia lebo yake ya NLM.

“Kuna sababu nyingi za Rayvanny kuondoka ndani ya WCB, nilizungumza naye akaniambia ni ishu ya asilimia anazopata, aliona amekuwa mkubwa sasa hivyo asilimia anazopata hazimtoshi tena kufanya mambo yake mengine.

“Pia alisema muda, kuna wakati anataka kufanya jambo kwa haraka lakini ikifika kwenye uongozi lazima lifuate mlolongo wa mchakato. Kwa mfano leo anaweza kupigiwa simu na Rihanna akafanye naye kolabo, akileta jambo hilo kwenye management zitaanza process pengine jambo litachelewa au lisifanyike. Yeye anataka akiwa na jambo lake, apande ndege aondoke, kifupi alitaka uhuru.

“Nachowashauri watu wenye lebo ni kwamba wasimsainishe msanii akiwa na njaa, wamuache ale ashibe kabisa ndipo wamsainishe, ukimsainisha mwenye njaa atasaini chochote tu kikubwa anataka kutoboa, akishakuwa mkubwa ndio ataona pesa haitoshi, anataka kuondoka na vurugu kama hizo," amesema Baba Levo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live