Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo: S2Kizzy naomba unisamehe

Baba Levo S2kizzy Baba Levo: S2Kizzy naomba unisamehe

Mon, 15 Aug 2022 Chanzo: Global Publishers

Ikiwa ni siku chache baada ya msanii na chawa wa Diamond Platnumz, Baba Levo kumshauri producer wa muziki, Salmin Kassim ‘S2Kizzy’ kuwa amshukuru Diamond kwa kumsaidia, msanii huyo aliibuka na kumtolea maneno makali Baba levo.

Sasa kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa msanii @officialbabalevo ameandika; "Nisamehe mdogo wangu S2Kizzy maana kitendo cha kunishambulia dm kimetosha kusema tukae mbali…!!!

“Najua sisi wote kuna siku @diamondplatnumz atatufukuza kama m’mbwa ila wewe haujafukuzwa s2kizzy …!! ila kama @diamondplatnumz hajakusaidia …!! narudia tena nisamehe maana naona unanilaumu bureee.

“Nilisema baada ya kumshukuru mungu mama na baba yako mshukuru na @diamondplatnumz coz amekusaidia kama hilo ni kosa basi nisamehe na naomba tuishie hapa maana mi nakuona kama hauna shukurani…!" amesema Baba Levo.

Chanzo: Global Publishers