Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo: Rayvanny ni mchawi.. Harmonize hamuwezi

Rayvanny Rayvanny Harmo Baba Levo: Rayvanny ni mchawi.. Harmonize hamuwezi

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa Bongo Fleva ambaye pia ni Official Chawa wa Diamond Platnumz, Baba Levo amesema kuwa Rayvanny ni msanii mkubwa na amejifunza vitu vingi kutoka kwa Diamond Platnumz, hivyo sio rahisi kwake kuporomoka kimuziki.

Baba Levo amesema kuwa, Vannyboy ndiye mchawi wa digital platforms ambapo Harmonize hawezi kumfikia hata kidogo.

“Rayvanny na Harmonize hawa wote wamejifunza maujanja kupitia kwa Diamond Platnumz, ni wajanja, Mondi aliwapa mbinu za kuweza kushindana kwenye game. Rayvanny ahwezi kuyumba sababu amekaa shule amejifunza vitu vingi sana kutoka kwa Diamond.

"Harmonize hamuwezi Rayvanny, usijidanganye, hamuwezi kabisa… Sababu Rayvanny ni mchawi wa Digital, ndiye anatengeneza pesa kubwa kwenye muziki wake kupitia digital platforms.

"Kuhusu Rayvanny kulipishwa na WCB Tsh milioni 50 sababu ya kufanya Tamasha la nandy huo ni uzushi na maneno tu ya kutengeneza. Sijaona sehemu ambayo Rayvanny amesema amelipishwa ama Diamond amesema amemlipisha Rayvanny," amesema Baba Levo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live