Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo: Rayvanny atakuwa msanii wa kwanza kuleta Tuzo ya Grammy Bongo

Rayvanny Srts Baba Levo: Rayvanny atakuwa msanii wa kwanza kuleta Tuzo ya Grammy Bongo

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa muziki nchini, Baba Levo amesema kuwa CEO wa NLM, Rayvanny ndiyo atakuwa msanii wa kwanza kuleta tuzo ya Grammy nchini Tanzania kwa sababu mtu aliyemshirikisha ni msanii mkubwa asiyezuilika.

Ngoma ya "Mama Tetema" (Maluma & Rayvanny) imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania Tuzo za Grammy kupitia Album ya Maluma iitwayo "Don Juan" katika kipengele cha "Best Latino Pop Album".

"Kama Rayvanny ataichukua tuzo ya Grammy na Diamond Platnumz atakua ameichukua mana huyo maluma asingeisikia tetema ya rayvanny bila diamond kuifanyia promotion," amesema Baba Levo

Mama Tetema ni track namba 21 katika album hiyo ya Maluma na producer S2Kizzy ndiye alitengeneza ngoma hii, hivyo na yeye yumo kama mtayarishaji wa wimbo huo.

Hii ni mara ya pili Kwa Rayvanny jina lake kuingia katika tuzo kubwa Duniani,. Mara ya kwanza alitajwa katika Tuzo za BET na alifanikiwa kunyakua tuzo.

Una maoni Gani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live