Msanii wa Bongo Fleva na mtangazaji wa Wasafi Media, Baba Levo amedai kuwa penzi la Paula na Marioo halitafika mwezi Desemba mwaka huu litakuwa limekufa.
Baba Levo amedai kuwa Marioo aatakuwa ameishiwa pesa kwani mrembo huyo yupo kwake kimaslahi zaidi na si kwa sababu ya upendo.
“Nachojua marioo na Rayvanny hawakuwa na vita yoyote ila vita italetwa na mwanamke, wakimgombania Paula ni vita ya kawaida tu.
“Namshauri Rayvanny, ameachana na Paula amechukuliwa na Marioo, kwani Marioo hana wanawake wengine ambao ameachana nao? Na yeye aende achukue kule, ni kuchukuliana tu, hata kama amerudi kwa mke wake hiyo ni michepuko tu.
“Marioo na Paula ni biashara, nawaambia penzi lao hawatafika mwezi Desemba, kuna mambo mawili, kwanza Marioo atakuwa ameishiwa na hela kabisa, ataanza kuwa ombaomba au ndugu yetu atapata mwanaume mwenye pesa nyingi zaidi.
“Niliona kwa Rayvanny alikuwa akiendesha gari anaongea peke yake sababu ameshapigwa mizinga na mtoto mpaka na mama, kwisha kabisa, alichanganyikiwa, nafurahi sasa namuona yupo na mkewe ni mwanamke mzuri,” amesema Baba Levo.