Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo: Mwijaku akawasemee Wanigeria

Mwijakuu Na Baba Levoo Baba Levo: Mwijaku akawasemee Wanigeria

Thu, 24 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CHAWA Pro Max mwenyewe anapenda kujiita hivyo ama Fundi Majumba, ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Baba Levo ameonesha kumpinga moja kwa moja mtangazaji wa Clouds Media, Burton Mwemba ambaye ameonyesha nia ya kuutaka usemaji wa Shirikisho la Muziki nchini (TMA).

Akizungumzia hilo, Baba Levo amesema Mwijaku hafai kabisa kuwepo kwenye kiti cha usemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania.

“Tuzo za BET mwijaku alikuwa mstari wa mbele kumpinga Diamond na kutaka watanzania wampigie kura Burnaboy aende akawasemee wa Nigeria,” alisema Baba Levo.

Ikumbukwe kuwa, Mwijaku alijitokeza hadharani kuutaka usemaji huo kufuatia mgogoro ulioibuka miongoni mwa wasanii wa muziki nchini baada ya Steven Mengere 'Steve Nyerere' kuteuliwa kuwa msemaji wao huku wengine wakimpinga na wengine wakimuunga mkono.

Licha ya Steve Nyerere kusema kuwa hang'atuki katika kiti hicho, hata hivyo Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) jana lilimzuia Steve kuendelea na majukumu yake ya usemaji mpaka mpaka pale ambapo litakapotoa maelekezo mengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live