Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo: Kujenga kwa sh elfu 75, kupanga siku ya kulewa ni umasikini

Mwanamke Hatongozwi, Anaalikwa Tu Baba Levo.png Baba Levo.

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Baba Levo amewachana watu wanaofikiria kila pesa wanayoipata ni kwa ajili ya kujenga au kufanya maendeleo badala yake amesema kuwa pesa nyingine wanatakiwa watumie kwa ajili ya kula na kufurahia maisha yao.

Baba Levo amedai kuwa, kitendo cha kufikiria kila pesa ni kwa ajili ya maendeleo hizo ni dalili za mtu masikini.

"Dalili ya kwanza ya umasikini ni kufikiria kujenga kwa hela ya kula. Unakuta mtu una shilingi elfu 75 unaanza kuwaza mambo ya ujenzi, hiyo ni hela unatakiwa ukae ule ujigalagaze.

"Na dalili ya pili ya umasikini ni kupanga siku ya kulewa/kunywa pombe, pombe haina siku maalum, inapangwa na hela zako kunywa muda wowote, ukiona umepanga siku maalum ya kunywa pombe ujue wewe ni masikini," amesema Baba Levo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live