Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo: Hakuna mtu mkandamizaji kwenye muziki kama P Funk

P Funk Baba Levoo Baba Levo: Hakuna mtu mkandamizaji kwenye muziki kama P Funk

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva ambaye pia ni Chawa wa Diamond Platnumz, Baba Levo amesema anamheshimu P Funk Majani kama legend wa muziki wa Bongo lakini hakupaswa kuishambulia biashara ya Wasafi kwani kama aliona kuna tatizo alipaswa kuzungumza katika maeneo sahihi ya kutolea maoni.

Kauli hiyo ya Baba Levo inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuibuka kwa sakata la Majani kudai kuwa WCB inawanyanyasa na kuwakandamiza wasanii wake hali inayopelekea kujiondoa katika lebo hiyo huku wakitakiwa kulipa mamilioni ya pesa.

“Mimi namjua P Funk miaka mingi, ni kaka, anapaswa kutoa maoni sehemu sahihi lakini ukitoa maoni sehemu si sahihi kwa lengo la kuwachafua ama kuharibu biashara zao, lazima watakulipua na wewe kukuchafua kama ulivyokuja, usiumie kwa sababu wewe ndio umeyachokonoa.

“P Funk ni legend kwenye muziki, ametengeneza ramani kuu ya muziki wa Bongo, heshima yake lazima apewe. Lakinini kuna wasanii wengi waliofanikiwa kupitia P Funk, lakini pia wapo wasanii kibao walioumia kupitia yeye, Diamond hawezi kusema lakini sisi tunaomzunguka tutamsemea.

“Tukisema tuwaanike mambo aliyowafanyia lazima ataumia. Ukiheshimiwa na wewe waheshimu wenzako, ukinitukana sokoni lazima name nitakujibu palepale sokoni ili watu wajue kwamba nimekujibu.

“Kusema WCB inakandamiza wasanii hiyo sio kweli, hakuna mtu mkandamizaji kwenye hii tasnia kama P Funk Majani, hakuna mtu amewanyanyasa watu kwenye hii Sanaa kama P Funk Majani, tunajua kwa sababu alikuwa na nguvu. Watu wamelalal nje ili tu kuongea naye, amewafukuza kama mbwa lakini haya yote hayafuti kazi kubwa aliyoifanya kwenye tasnia,” amesema Baba Levo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live